SINGIDA BIG STARS WANAGAWA DOZI TU - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 3 December 2022

SINGIDA BIG STARS WANAGAWA DOZI TU


 MABAO matatu ambayo yameituliza Namungo FC ikiwa Uwanja wa Majaliwa yamefungwa na nyota watatu ambao kwa nyakati tofauti wote waliwahi kucheza mitaa ya Kariakoo.


Ubao wa Majaliwa Desemba 2,2022 ulisoma Namungo 0-3 Singida Big Stars na kuwafanya vijana wa Hans Pluijm kusepa na pointi tatu ugenini.


Ni Meddie Kagere alikuwa wa pili kufunga bao la pili dakika ya 76 na wa kwanza kufunga alikuwa Said Ndemla dakika ya 27.


Shukran kwa Amis Tambwe ambaye alifunga bao la tatu kukamilisha idadi hiyo kwa wakulima hao dakika ya 90+2.


Jithada za Namungo kusaka ushindi zilikwama licha ya uwepo wa mashabiki wao.


Ni bao la nne kwa Meddie Kagere msimu huu akiwa na uzi wa Singida Big Stars baada ya kusepa ndani ya kikosi cha Simba baada ya msimu wa 2021/22 kumeguka.


Ukitazama msimamo sasa Singida Big Stars ni nafasi ya nne baada ya kucheza mechi 14 na pointi zao ni 27, Namungo FC ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 14.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad