TAMBO ZATAWALA DABI YA KARIAKOO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 21 December 2022

TAMBO ZATAWALA DABI YA KARIAKOO


 KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa dabi ya Kariakoo upande wa Wanawake, Simba Queens v Yanga makocha wote wameweka wazi kwamba wapo tayari kwa mchezo huo.


Simba Queens ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Wanawake Tanzania watawakaribisha Yanga Princess Uwanja wa Mkapa.

Kocha Mkuu wa Yanga Princess ambaye ameibuka hapo muda mfupi baada ya kuacana na mabosi zake wa zamani Simba Queens ameweka wazi kuwa hautakuwa mchezo rahisi:-“Hautakuwa mchezo rahisi kwa timu zote mbili, nilikuwa mwalimu wa Simba Queens na ninawafahamu wachezaji wao na wao wananifahamu, hivyo hautakuwa mchezo mwepesi,".

Kwa upande wa Charlses Lukula, Kocha Mkuu wa Simba Queens amesema kuwa wanatambua mchezo hautakuwa mwepesi wapo tayari kwa ajili ya kupata ushindi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad