BAADA ya kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumshambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na wapembeni Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ataibukia kwenye Uwanja wa Mkapa mchezo dhidi ya Coastal Union.
Yanga ndani ya Desemba ina vigongo 7 ambapo Nabi kafungiwa kwenye
mechi tatu kutokana na kosa hilo hicyo ni Cedric Kaze, kocha msaidizi wa Yanga
atakuwa kwenye benchi la ufundi.
Vigongo 7 kwa Yanga ndani ya dakika 630 ni mechi nne
watakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa huku tatu wakiwa ugenini.
Kazi inatarajiwa kuanza Jumapili, Desemba 4 ambapo Yanga
itamenyana na Tanzania Prisons, mchezo ujao itakuwa ni Namungo v Yanga, Desemba
7.
Yanga v Kurugenzi huu ni mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya
Pili unatarajiwa kuchezwa Desemba 9/11, Yanga v Polisi Tanzania, Desemba 17
kigongo kingine ni Yanga v Coastal Union, Desemba 20 hapa adhabu ya Nabi
itakuwa imemeguka.
Vigogo hao watakutana na vigongo wenzao Azam FC itakuwa
Desemba 25 siku ya Sikukuu ya Christmas na kigongo cha mwisho itakuwa dhidi ya
Mtibwa Sugar, Desemba 31 ambapo shughuli ya Desemba itafungiwa Uwanja wa
Manungu, Morogoro.
Nabi hivi karibuni aliweka wazi kuwa ratiba ni ngumu
kwao lakini wanapambana kutafuta matokeo chanya.
“Ukitazama ratiba kweli ni ngumu hilo lipo wazi na niliwaambia
tangu mwanzo lakini sio sababu kwamba tukikosa matokeo iwe ni kigezo hapana,
tunafanya maandalizi kutafuta ushindi kwa kila mechi,”.

No comments:
Post a Comment