MZAWA Dickosn Job anayekipiga ndani ya kikosi cha Yanga ameweka rekodi yake matata kwa kuwa mzawa pekee ambaye amefunga kwa timu za Kariakoo Februari ndani ya Uwanja wa Mkapa.
Mechi
za ufunguzi wa Februari, Simba na Yanga zote zimecheza Uwanja wa Mkapa na kusepa
na ushindi ilianza Simba Februari 3 ubao uliposoma Simba 3-1 Singida Big Stars.
Kwenye
mchezo huo mabao ya Simba yote yalifungwa na wageni ilikuwa ni Jean Baleke wa
Dr Congo, Saidi Ntibanzokiza wa Burundi hawa walitumia pasi za Clatous Chama wa
Zambia na Pape Sakho kutoka Senegal aliyetumia pasi ya beki mzawa Shomary
Kapombe.
Hata
bao la Singida Big Stars lilipachikwa na Bruno Gomez ambaye ni raia wa Brazil
hivyo kwenye mabao manne yaliyofungwa hakuna mzawa aliyefunga zaidi ya pasi
moja ya Kapombe.
Job
alivunja mwiko huo kwa kupachika bao moja Februari 4 ubao uliposoma Yanga 2-0
Namungo FC akitumia pasi ya Djuma Shaban ambaye alipiga kona Uwanja wa Mkapa na
bao la pili lilifungwa na Aziz KI.
Kwenye
mabao sita ambayo yamefungwa Uwanja wa Mkapa, mzawa mmoja tu kafunga ambaye ni
Job na kwa pasi pia ni mzawa mmoja katoa ambaye ni Kapombe wa Simba ndani ya
ligi.
No comments:
Post a Comment