KUTABIRIKA kwa matokeo hakuna kwenye ulimwengu wa soka kutokana na kila timu kujipanga kwa umakini kupata ushindi.
Iwe ni nyumbani ama ugenini kwa sasa kila timu ina nafasi ya
kupata matokeo hasa kwenye mechi za kimataifa ambazo ufuatiliaji wake huwa ni
kwa ukaribu.
Wale ambao hawajaanza maandalizi kwenye mechi za kimataifa kwa
sasa kazi ni kubwa kwa kuwa ni muhimu kufanya maandalizi mazuri kwa sasa.
Wawakilishi kutoka Tanzania ambao ni Yanga na Simba wana kazi
kubwa ya kufanya kwenye mechi zote ambazo zinawahusu.
Kikubwa ni kupeperusha bendera kwa umakini kwenye mechi ambazo
zinawahusu hasa kwenye hatua ya makundi ambayo ushindani wake ni mkubwa.
Ambacho kinatazamwa ni pointi tatu kwa namna kasi ilivyo na
ushindani ulivyo kwa timu ambayo haitafanya maandalizi mazuri maumivu
itaambulia.
Simba wao wapo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku kazi ni kubwa
kuwania kutinga hatua ya robo fainali kisha hatua ya nusu fainali mpaka
fainali.
Hata Yanga pia kwenye Kombe la Shirikisho kazi ni moja kusaka
pointi tatu kwenye mechi ambazo mtacheza.
Ili kushinda kimataifa mbinu bora na wachezaji kujituma bila
kuogopa inahitajika na hilo lipo kwenye miguu yenu kwa sasa.
Dakika 90 za kimataifa iwe ni ugenini ama nyumbani ziwe za kazi
kubwa na nzuri kusaka ushindi ili kuongeza nafasi ya timu shiriki kimataifa.
No comments:
Post a Comment