KILA mmoja anafuata njia zake ambazo zitampa mafanikio akikwama kidogo kupotea ni hatua inayofuata asipojipanga itakuwa kazi nyingine.
Ilikuwa hivyo Uwanja wa Liti, njia za Sigida Big Stars wakulima wa
alizeti njia ziliwagomea na zile za Yanga zikawapa ushindi baada ya dakika 90.
Ngoma fainali ya Azam Sports Federation itakuwa ni Azam FC v
Yanga, Tanga, hapa tunakuletea namna njia zizivyochorwa namna hii:-
Metacha Mnata
Aliibuka Yanga akitokea Singida Big Stars kwenye dirisha dogo na
ameanza kazi katika mchezo dhidi ya mabosi wake wa zamani alikaa langoni.
Ni hatari dakika ya 9, 51 aliokoa alichezewa faulo dakika ya 21 na
Franciy Kazad ambaye alionyeshwa kadi ya njano ya kwanza na alimchezea faulo
kwa mara nyingine dakika ya 76 alisepa na dakika zote 90.
Djuma Shaban
Shuhuda wa timu ya Yanga ikitinga hatua ya fainali Azam Sports
Federation huku ukuta wao ukiwa haujatunguliwa ugenini.
Joyce Lomalisa
Mwamba huyu alichezewa faulo dakika ya 45 katika mchezo huo
uliokuwa na matumizi makubwa ya nguvu mwanzo mwisho.
Bakari Mwamnyeto
Nahodha mzawa Nondo alionyesha kazi yake akiokoa hatari dakika ya
65 alikutana na mkato wa kimyakimya dakika ya 59.
Ukuta wao haukuruhusu kutunguliwa kwenye mchezo huo wa hatua ya
nusu fainali ya pili.
Mamadou Doumbia
Beki wa kazi aliokoa hatari dakika ya 8, 9, 12, 50, 53, 55
alikwama kusepa na dakika 90 alisepa na dakika 64 Dickson Job aliingia
kukamilisha ngwe iliyobaki.
Zawadi Mauya
Kiungo Mauya alisepa na dakika 90 mazima akiokoa hatari dakika ya
45 na muda aliotoka Doumbia alirejea nyuma kuongeza nguvu ya ulinzi mpaka
alipoingia Job kukaa kwenye eneo lake.
Jesus Moloko
Moloko ni miongoni mwa nyota waliokuwa na shauku ya kulisaka lango
la Haule, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 59. Alikuwa anakula sahani
moja na Shafiq Batambuze aliyeoonyeshwa kadi ya njano dakika ya 38.
Alisepa na dakika 77 aliingia mzee wa spidi 120 wakumuita Tuisila
Kisinda ambaye alikamlisha dakika zilizobaki.
Salim Aboubhakari, ‘Sure Boy;
Kiungo wa kazi alipiga kazi eneo lake akiwa na kazi ya kupiga
krosi kama alivyofanya dakika ya 63 Uwanja wa Liti.
Clement Mzize
Kagotea kwenye mabao sita kwenye mashindano haya na bado mchezo
mmoja wa fainali dhidi ya Azam FC.
Kwenye eneo la ushambuliaji alichezewa faulo dakika ya 10 alipiga
shuti ambalo lililenga lango dakika ya 22 alisepa na dakika 77 aliingia Kennedy
Musonda aliyekuwa akipambana na Pascal Wawa aliyeokoa hatari dakika ya 65, 66
na alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 61, 65..
Aziz KI
Kiungo wa kazi Aziz KI alianza kikosi cha kwanza alipiga faulo
dakika ya 9, 72 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 27, 30, 53,
alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 53.
Ni dakika 77 alisepa nazo akaingia Fiston Mayele ambaye
alipachika bao dakika ya 82 akiwa ndani ya 18 alipomtungua Haule bao pekee la
ushindi.
Farid Mussa
Kiungo
Farid Mussa alipiga krosi dakika ya 63 alisepa na dakika 64 ngoma ilichukuliwa
na Dennis Nkane kwenye mchezo huo.
Nyota
huyo alikuwa kwenye eneo la kiungo kama Aziz Andambwile ambaye alionyeshwa kadi
ya njano dakika ya 64.
No comments:
Post a Comment