GANZI YA MAUMIVU ILIANDIKWA MIKOA ZAIDI YA MIWILI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 20 January 2024

GANZI YA MAUMIVU ILIANDIKWA MIKOA ZAIDI YA MIWILI

 


ILE simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo iliyokuwa ikiandikwa gazeti la Championi Jumatano visa vyake viliandikwa kwenye mikoa zaidi ya miwili Tanzania kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii husika.

 

Ipo wazi kwamba simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo inaingia kwenye orodha ya simulizi bora zilizopata nafasi ya kuchapishwa ndani ya gazeti la Championi Jumatano ikiwa ni utunzi wa Lunyamadzo Mlyuka.

 

Kwa sasa mchakato unaendelea kufanyia kazi maombi ya wasomaji kupatikana kitabu kinachotarajiwa kutoka hivi karibuni na oda kutoka sehemu mbalimbali zimeanza kutolewa ikiwa ni pamoja na Lindi, Njombe, Kibaha, Arusha, kuna nafasi ya kutoa oda pamoja na udhamini.

 

Akizungumza kuhusu mikoa iliyopata nafasi ya simulizi hiyo kuandikwa kwa nyakati tofauti na visa vikapatikana, Mlyuka alisema: “Kuna sehemu mbalimbali ambazo zimejumuishwa ndani ya simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ikiwa ni Mtwara, Kibaha, Arusha, Iringa, Njombe kwa lengo la kuongeza ladha na simulizi kuwa kwenye ubora wake.

“Ina visa vingi vya kuvutia na kusisimua hivyo sio kazi ya kuikosa kwa kuwa inatoa elimu kuhusu maisha halisi tuliyopo kwa sasa, furaha, huzuni yale yote yanayoifanya dunia izunguke yapo kwenye simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo,”.

 

Kwa oda, udhamini wasiliana moja kwa moja na mwandishi 0756 028 371. Kwa sasa simulizi inayoendelea ni Msichana wa Maisha Yangu, ndani ya Championi Jumatano.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad