KUVUNJIKA kwa koleo sio mwisho wa uhunzi ipo hivyo ni lazima kazi iendelee kwa kuwa haiwi mwisho mpaka ifike mwisho hivyo tu basi.
Tumeona namna mwanzo usiofurahishwa kwa timu ya taifa ya Tanzania kwenye Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Morocco.
Kila mmoja ana jambo lake kutokana na hali halisi kuwa kutokuwa kwenye mwendo mzuri wa timu kupata matokeo na mwisho kupoteza mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi.
Ni muda wa kufanyia kazi makosa yaliyopita ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinzofuata kwa kuwa kila timu inahitaji kupata ushindi kwenye mechi ambazo inashuka uwanjani.
Tumeona namna ambavyo kila timu inafanya vizuri inaposhuka uwanjani kutafuta ushindi ndani ya dakika 90 ipo hivyo na inatakiwa kuwa hivyo mwanzo mwisho.
Muda ni sasa kwenye mechi ambazo zimebaki wachezaji kufanya kweli kwa kutengeneza nafasi na kuzitumia kujilinda inatosha ni muda wa kutafuta ushindi.
Nidhamu ni muhimu pia kuongezekana kwa kuwa tumeona mchezo wa kwanza ulitugharimu kwa kadi nyekundu na mwisho kila mmoja anakazi kutimiza majukumu yake.
Pongezi kwa mashabiki ambao mnazidi kuwa pamoja na timu Ivory Coast, hakuna mkataba wa kunyoosha mikono ni mwendelezo wa kutafuta ushindi.
Kila la kheri kwenye mechi zijazo inawezekana kupata ushindi na muda ni sasa kwa kuwa kila kitu kinawezekana.
No comments:
Post a Comment