MLANDEGE wameendeleza ubabe wake kwa ushindi wa bao 1-0 Simba katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Amaan.
Katika fainali ya Mapinduzi 2024 Mlandege waliingia kwa mbinu ya kujilinda zaidi kipindi cha kwanza na kuwavuruga wachezaji wa Simba waliokuwa wakiliandama lango la wapinzani wao kutafuta bao la kuongoza.
Ngoma ilikuwa nzito kipindi cha pili ambapo Joseph Akandwanao aliwakanda Simba dakika ya 54 ya mchezo aliposepa na kijiji cha mabeki wawili wa Simba waliokwama kumzuia nyota huyo.
Bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na Simba ikipoteza mchezo wake wa kwanza katika hatua ya fainali huku Mlandege wakishinda mchezo mmoja ambao ni wa fainali.
No comments:
Post a Comment