DOLA milioni 25 kwenye akaunti, zaidi ya bilioni 50 za kitanzania zimetulia.
Sadio anayaishi maisha ya starehe, kwenye dunia yenye vingi vinavyofurahisha macho.
Nani anasema pesa sio kila kitu, atuambie kauli yake anaitoa akiwa na bei gani tigopesa...!? Mwambieni Sadio ana hela, anaishi vizuri, na juzi Kaongeza furaha nyingine.
Yupo salama sana, mwanaume mwenye mwanamke wa ndoto zake pembeni. Kwenye ndoa na binti wa miaka 18, tarehe 7 kasema haanzi mashindano ya Afcon, kama Aisha hajawa mke wake wa halali.
Atarudi akiwa amechoka, atakasirika wakiwa wamefungwa, atakutana na Aisha mwenye amani yake. Atalikosa kombe, bado utamu wa ndoa mpya, utampokea kwa kumbato linalomaanisha.
Watabeba ubingwa, ataenda kumalizia honeymoon nchi anayoitaka, akiwa na medali shingoni, atake nini tena. Sadio kwenye ndoa yake na Aisha, kuna mwamba huku Magomeni, kashaachana na wanawake 270 hadi sasa.
Sadio anatufundisha uliekula nae tembele, jitahidi ukizipata, Pizza achague yeye. Uliemshikia bomba kwenye daladala, ukinunua Crown ya ndoto yako, awe kushoto akibadilisha amapiano anayoitaka.
Vijana mnaingia mwaka mpya na pisi mpya, kila siku unajiona una mkosi, kumbe una machozi yenye jina lako kila mtaa.
Ameandika Kaisal Ally
No comments:
Post a Comment