SINGIDA FOUNTAIN GATE WAIGOMEA AZAM FC - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday 8 January 2024

SINGIDA FOUNTAIN GATE WAIGOMEA AZAM FC


 NIZAR Khalfan, kocha msaidizi wa Singida Fountain Gate ameweka wazi kuwa hawatakubali kupoteza kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Azam FC, unaotarajiwa kuchezwa leo Januari 8 2024.

Ikumbukwe kwamba mwaka mmoja uliopita tarehe kama ya leo ilikuwa ni robo fainali kwa wababe hawa wanaokutana kwa mara nyingine ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC 1-4 Singida Fountain Gate.

Mabao ya Singida Fountain Gate yalifungwa na Francy Kazadi huku lile la Azam FC likifungwa na Abdul Suleiman, (Sopu) ambaye hajawa na nafasi kikosi cha kwanza kwenye mechi za hivi karibu.

Khalfan ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wataingia kwa nidhamu ili kupata matokeo kwenye mchezo huo.

“Tunatambua mchezo utakuwa mgumu lakini hatutakubali kupoteza mchezo wetu dhidi ya Azam FC. Tunawaheshimu na tunajua kwamba wamekuwa kwenye mwendo mzuri katika mechi wanazocheza.

“Wachezaji wapo tayari tunaamini utakuwa ni mchezo wenye ushindani hasa ukizingatia kwamba Azam FC watakuwa wanahitaji kulipa kisasi,” alisema Khalfan.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad