MOJA ya mechi bora katika Mapinduzi Cup hii hapa Jamus FC 1-2 Yanga zilikuwa dakika 90 zenye ushindani mwanzo mwisho ambapo pointi tatu zilikuwa mali ya Yanga.
Farid Mussa alifungua pazia la mabao dakika ya 16 liliwekwa usawa na David Clement dakika ya 42 akitumia makosa ya ulinzi ya Yanga walipoacha nafasi kwa kwenda mbele kutafuta bao lingine.
Nickson Kibabage jioni alifunga bao la ushindi dakika ya 90+7 akitumia pasi ya Clement Mzize.
Leo Januari 3 ni APR v JKU saa 10:15 kisha Simba SC v Singida Fountain Gate saa 2:15.
No comments:
Post a Comment