MASHUJAA KAMILI KUWAVAA DODOMA JIJI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday 11 February 2024

MASHUJAA KAMILI KUWAVAA DODOMA JIJI

 


BAADA ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Mashujaa FC wameweka wazi kwamba mpango wao ni kupata pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji.

Ipo wazi kwamba Februari 8 2024 ubao wa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ulisoma Yanga 2-1 Mashujaa ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa timu hiyo kupoteza kwa kuwa awali ilipoteza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ukisoma Mashujaa 0-1 Simba.

Leo Februari 11 itakuwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kusaka pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji ambao nao mchezo wao uliopita walipoteza ka kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, Uwanja wa AzamComplex.

Abdallah Mohamed, (Bares) Kocha Mkuu wa Mashujaa amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa na malengo ni kupata pointi tatu kwenye mchezo huo.

"Tunatambua mchezo utakuwa mgumu na wapinzani wetu wapo imara lakini malengo yetu ni kupata pointi tatu tuna amini itakuwa hivyo na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mapambano,".

Kwenye mechi hizo mbili mfululizo langoni alianza kipa namba Eric Johora ambaye aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Yanga.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad