Disco toto Marufuku Dar - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 9 December 2016

Disco toto Marufuku Dar


JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam limepiga marufuku disko toto kipindi cha sikukuu ya Maulidi na kuwataka wazazi kuwa karibu na watoto wao kipindi hicho ili kuhakikisha usalama wao.
Akizungumza
Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Simon Sirro
 Dar es Salaam, Kamishna wa kanda hiyo Simon Sirro alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga kuhakikisha siku hiyo inakuwa ya utulivu zaidi.
“Tumejipanga na kutakuwa na makachero kila kona, doria za miguu, askari kanzu, askari wa mbwa na farasi, jeshi la kuzuia fujo (FFU) na magari ya doria ili kuhakikisha amani na usalama unatawala kila mahali,” alisema Sirro.
Kamishna Sirro aliwataka wazazi na walezi kuwafunza watoto wao maadili mema ili kujiepusha kuwa katika makundi mabaya kama Panya road, ulevi na vurugu kwa kipindi hicho,
 “Wazazi tuwalinde watoto wasizurule ovyo pia tukielekea maeneo ya starehe nyumbani tuache ulinzi wa uhakika,” alisema.
Katika hatua jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sugu 103 wa makosa mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa kipindi cha kuanzia Desemba 2 hadi 8 mwaka huu.
Makosa hayo ni pamoja na kucheza kamari, wizi wa magari, kutengeneza kunywa na kuuza pombe haramu ya Gongo, na kueleza kuwa oparesheni hiyo itakuwa endelevu.
Pia jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalum ya Dar es Salaam wamefanikiwa kukusanya zaidi ya sh. Milioni 400 kupitia tuzo za makosa ya kiusalama barabarani,

Kiasi hicho kimepatika kwa kipindi cha kuanzia Desemba 2 hadi 7 mwaka huu ambapo jumla ya makosa 15,053 yalikamatwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad