Balozi wa Japn afungua mashindano ya baseball - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 9 December 2016

Balozi wa Japn afungua mashindano ya baseball


BALOZI  wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida amefungua rasmi mashindano ya taifa ya mchezo wa baseball na softball unaozihushisha timu saba za mikoa mbalimbali nchini Tanzania yenye lengo la kupata timu nzuri ya taifa itakayoshiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo mwaka 2020
Balozi wa Japan Nchini Tanzania Masaharu Yoshida (Kulia)
Akizindua mashindano hayo Dar es Salaam amesema kuwa anafurahi kuwa miongoni mwa watu muhimu kaika ufunguzi wa mashindano ya mchezo huo ambao ni maarufu sana nchini Japan na kuahidi kutoa ushirikiano mzuri ili kuleta maendeleo ya mchezo huo nchini
“Serikali ya Japan inaahidi kuwa bega kwa bega katika kuhakikisha kuwa mchezo wa baseball unapiga hatua na tunaahidi kujenga uwanja wa mazoezi katika shule ya sekondari ya Azania utakaopewa jina la “Koshien” ambayo ni sehemu ambapo mechi za timu za shule za ngazi ya juu Japan huwa zinachezwa”alisema.
Aidha alisema kuwa anapata faraja kuona mashindano ambayo yanawahusisha wachezaji vijana waliojifunza na kujiandaa wakiwa  wenye morali na nguvu kwa ajili ya kushindana na kuwatakia kila la kheri katika mashindano.
 Katibu Mkuu  wa Chama cha Baseball na Softball Tanzania (TaBSa) Alpherio Nchimbi alisema kuwa timu zimewasili salama  na mashindano yameshafunguliwa rasmi hivyo  na kila kitu kinakwenda sawa na kuwasihi wadau waweze kujitokeza kuyatazama mashindano hayo yanayowahusu wanafunzi wa sekondari.
“Mashindano yameshafunguliwa rasmi ambapo timu saba ndizo zipo kwenye makundi na timu zilizofungua pazia la mashindano ni  Kibasila na Juhudi,ushindani uliopo ni mkali na hii inaleta hamasa na tunaamini tutapata timu ya taifa yenye ubora ambayo itaiwakilisha vema Tanzania katika mashindano ya kimataifa “alisema.
Alisema kuwa mashindano hayo yaliyopewa jina la Uhuru Cup yanaongozwa na kauli mbiu inayosema  Uhuru na kazi kwa kuwa michezo ni elimu na ajira hivyo amewataka watanzania kuwekeza pia kwenye mchezo wa Baseball ambao nao ni sehemu ya michezo inayofuatiliwa duniani
Mohamed Pazi Mwalimu wa Juhudi sekondari amesema kuwa ni wakati wa wazazi na walezi kutumia fursa hii kwa kuwaruhusu watoto kushiriki kwenye michezo wawapo mashuleni kwa kuwa michezo ni afya pia ni sehemu inayowakutanisha watu mbalimbali na kuongeza urafiki na mahusiano baina ya wanamichezo.
“Watoto wapewe ruhusa kushiriki michezo mbalimbali wakiwa shuleni hata kipindi cha likizo kwa kuwa hii ni fursa ya kuwapatia watoto ajira na kuwaimarisha kiafya zaidi kwa mafunzo wanayoyapata wakiwa kambini”,alisema.
Mashindano hayo yana zihusisha timu kama Azania,Kibasila na Juhudi za Dar Es Salaam,Iyunga ya Mbeya,Sanya juu ya Kilimanjaro,Mwanakwereke C ya Zanzibar,Kombaini ya Mwanza,Dodoma yanafanyika katika viwanja vya Azania.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad