WANANCHI
wametakiwa kujitokeza katika maonesho la wazi linalojumuuisha makundi yote
yaliyo katika sekta ya kilimo ambao ni pamoja na wakulima,wafugaji ,wavuvi na
wawindaji yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chuo kikuu cha Dar es
Salaam kuanzia desemba 22 hadi 24 mwaka huu.
![]() |
| Dr Vincesia Shule (kulia) akifafanua jambo kuhusu mkulima market |
Akizungumza
Dar es Dar es Salaam Vincesia Shule Mwandaaji wa maonesho hayo alisema kuwa
lengo la kufanya shughuli hiyo ni kuhakikisha wanatoa fursa na upatikanaji wa
soko kwa wajasiriamali wadagowadogo na kuwawezesha wananchi kuziona bidhaa
zinazozalishwa na wakulima na hakutakuwa na kiingilio.
“Tunatoa
fursa kwa wakulima kuweza kupata soko la uhakika na kutafuta suluhu za
wajasiriamali katika kuwa wabunifu zaidi ili waweze kujikwamua kwa kupitia
bidhaa zao pamoja na kuwapa ujuzi wa namna ya kuzalisha bidhaa zinazoendana na
uhitaji pamoja na kupata nembo ya ubora ya TBS kwenye bidhaa zao”alisema
Aidha
aliongeza kwa kusema kuwa wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali ili kuweza
kuwafikia wakulima na kuwapa taarifa zinazohusu upatikanaji wa masoko na bidhaa
kwa wakulima kupitia vyombo vya habari ili kuweza kuimarisha ushindani katika
masoko mbalimbali.

No comments:
Post a Comment