Maharamia wabumisha soko bongo Movie - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 12 January 2017

Maharamia wabumisha soko bongo Movie

WASANII wametakiwa kuwa wabunifu  na kushirikiana katika tasnia ya filamu ili waweze kurudisha soko ambalo limeonekana kuanza kuyumba .
Katibu wa chama cha wasanii Mkoani Pwani (TDFAA) Kadnas Nassir alisema kuwa bado wana nafasi ya kurejesha heshima sokoni.
“Tukiwa wabunifu zaidi kwa kucheza sinema zenye maadili zinazozungumzia jamii tunauwezo wa kurudi kwenye ramani na kufanya vizuri hadi ngazi za kimataifa”alisema Nassir
Alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazoua soko mtandao unaotafsiri filamu za kigeni kwa kuweka maneno ya kiswahili hali inayodororesha soko na kupoteza mapato kwa serikali .

“Hawa wanaotafsiri wanachukua filamu kwenye mtandao ni maharamia kwa kuwa hawalipi kodi ila kazi tunalipia kodi hivyo mashabiki wathamini vitu vya ndani kwa manufaa ya taifa”alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad