Darrassa Usivimbe Kichwa - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 12 January 2017

Darrassa Usivimbe Kichwa


MSANII wa muziki wa kizazi kipya kwa mtindo wa “Hiphop” ametakiwa kutobweteka kutokana na kuwa gumzo midomoni mwa watu pamoja na nyimbo zake kupigwa kila kona.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam mashabiki wamesema kuwa kwa kukubalika huko yampasa kufanya kweli na kuongeza juhudi ili abaki kileleni.

 Christina Anold ambaye ni mwanamitindo amesema kuwa afanye mithili ya mashairi yake yanavyosema katika wimbo wake wa maisha na muziki atazidi kufanya vizuri.

“Amesoma muziki na kujua mashabiki wanataka nini akisimamia pale anposema kazi juu ya kazi hatasahulika atazidi kuongeza mashabiki na kuendelea kung’ara kwenye fani ila asibwete na umaarufu”alisema Christina.

Hassani Mpate ambaye ni msanii wa filamu alisema kuwa mafanikio ya muda mfupi ayakatae badala yake aongeze juhudi ili awe wa kimataifa katika fani ya muziki.

“Mashairi yake mwenyewe yanamfunga kwa mfano anasema usipotembea utabebwa mgongoni akijisahau tu mashairi yamhukumu na mashabiki watamsahau”alisema Mpate.


Nyimbo tatu alizoziachia kwa mpigo ambapo kama ingekuwa kwenye mpira ingeitwa “hat trik” Kama utanipenda na Too much zimepokelewa vema huku ile ya muziki ukiendelea kubamba mtaani na kuwa kama wimbo wa taifa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad