Jeshi la polisi labebeshwa zigo la lawama - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 13 January 2017

Jeshi la polisi labebeshwa zigo la lawama



MADEREVA wamelitaka jeshi la polisi kutowekeza nguvu nyingi kukusanya mapato kwa wale wanaofanya makosa kwani wamekuwa wakitozwa hata makosa yanayostahili kuonywa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Dar es Salaam wamesema kuwakuna haja ya kuwapa nafasi wamiliki wa vyombo vya moto kupewa elimu zaidi pale wanapokosea.
Kamanda wa Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Simon Siro
Imamu Juma ambaye ni dereva alisema kuwa wamekuwa na tabia ya kuwavizia ili kubaini makosa ya barabarani.
“Unaweza kuwa upo barabarani ghafla polisi anatokea mbele na kuonesha ishara ya kukusimamisha hali inayoleta taharuki kwa waendesha magari”alisema
Hassan Ally
ambaye dereva wa bodaboda alisema kuwa kitengo cha elimu yakipasa kifanye kazi kwa kuweza kufafanua juu kuweza kusaidiana kupunguza ajali na sio kuwatonza faini.
Kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam,Simon Sirro alisema kuwa wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo madereva yawapasa kutambua hilo na kutii bila shuruti.
“Kuna makosa mengine ambayo yakitokea jeshi la polisi tunatumia nafasi kuwaonya na wengine hutonzwa faini pia wengine hupelekwa mahakamani hivyo yawapasa kutii sheria”alisema Sirro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad