Mfuko awafunda Vijana - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 11 February 2017

Mfuko awafunda Vijana


VIJANA 50 walio nje ya shule wamefundishwa elimu ya uzazi na kujilinda na maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na mimba za utotoni ili kuwafundisha wengine.

Mkurugenzi wa UNA Steve Mfuko
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Mkurugezi wa UNA  (Uigizaji Ngoma Asilia) Steven Mfuko alisema kuwa wameamua kutoa mafunzo kwa vijana ili kukuza ufahamu
wao kuhusu masuala ya afya.

“Tunatoa mafunzo kwa vijana kuanzia miaka 12-23 kwa kuwafunza masomo ya afya ya uzazi pamoja na mbinu za kujilinda dhidi ya magonjwa ya zinaa ambayo yamekuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo”alisema

Alisema kuwa wameamua kutoa elimu kwa vijana ili kuwapa ujuzi wa kutosha na kwa wale watakaopata mafunzo wanajukumu la kuwafunza wengine ili ujuzi usipotee.

“Elimu ni silaha pekee itakayosaidia kuokoa jamii kutoka katika giza la kutokujua kuhusu elimu ya afya pamoja na magonjwa ya zinaa ambayo yamekuwa chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI”alisema Mfuko.

Rajabu Hamis ambaye ni mwanafunzi katika mradi huo alisema kuwa wanafundishwa mbinu mbalimbali kuhusiana na kirafiki zaidi juu afya ya uzazi hali inayowafanya waweze kuelewa masomo yanayoendeshwa na asasi hiyo.


“Tunafundishwa na walimu wenye uzoefu na waliobobea katika sekta ya afya hali inayotufanya tuweze kuelewa masomo pamoja na kufurahia darasa”alisema Hamisi 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad