Victor Denis
Dar es Salaam
RAIS wa serikali ya
wanafunzi katika chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DASJOSO) Lunyamadzo Mlyuka amewataka wanafunzi kutumia muda wao kuwa na
nidhamu katika matumizi ya muda kwani mafanikio ndipo yalikofichwa.
Akizungumza na wanafunzi hao chuoni hapo alisema kuwa kutumia muda kwa ufasaha kunaweza kumfaya mwanafunzi akawa na uwezo mkubwa kwani wote waliofanikiwa walikuwa makini kwenye matumizi ya muda.
![]() |
| Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DASJOSO) |
“Mafanikio yanabebwa na nidhamu hasa kwa kuweza kujali muda
pamoja na kujituma kwa juhudi isiyo ya kawaida hali itakayofanya kuwa tofauti
katika shughuli zinaweza kuleta mabadiliko chanya kwa kila mwanafunzi”alisema.
Aidha aliwataka wanafunzi kuongeza juhudi na kutumia nguvu
iliyojificha ili kukamilisha katika kujifunza kwa kuhakikisha kuwa wabunifu
katika tasnia ya uandishi kwa ni kuna ulazima wa kutambua wanakamilisha malengo.
"Kuna haja kufuata sheria na taratibu ikiwa ni
pamoja na kulipa ada kwa wakati ili kuingia kwani hakuna mwanafunzi anayeweza
kufundishwa iwapo hajakamilisha ada hivyo tuna wajibu wa kutiza hilo bila
shurti”alisema..
Japhary Lesso ambaye ni mwanafunzi wa ngazi ya cheti alisema
kuwa ugumu upo kwa upande wa ratiba kupuuzwa kwani wamekuwa wakishindwa
kuendelea na masomo hali ambayo inawaumiza kwa muda mrefu.

No comments:
Post a Comment