AUBA MAJANGA HUKO,HAIJAFAHAMIKA ITAKUWAJE JUMAMOSI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 18 November 2021

AUBA MAJANGA HUKO,HAIJAFAHAMIKA ITAKUWAJE JUMAMOSI

 


NYOTA wa Arsenal, Pierre Aubameyang inawekana akaukosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool unaotarajiwa kuchezwa Novemba 20, Uwanja wa Anfield kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Nyota huyo aliumia akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Gabon ilipokuwa kwenye harakati za kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia na timu yake ya Arsenal ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 11.

Auba alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Misri uliochezwa Jumanne na timu yake ilinyooshwa kwa kufungwa mabao 2-1 na inaelezwa kuwa nyota huyo amepata majeraha na kwa sasa yupo chini ya uangalizi ili kuweza kufahamu tatizo ambalo linamsumbua.

Pia hata Jurgen Klopp Kocha Mkuu wa Liverpool ambayo ipo nafasi ya nne na pointi 22 wapo nyota wake ambao atawakosa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Sadio Mane ambaye naye aliumia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad