DICKOSN JOB BABA LAO YANGA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 18 November 2021

DICKOSN JOB BABA LAO YANGA

 


MZAWA Dickosn Job mali ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi anakimbiza kwenye suala la dakika kwa kuwa akianza anakaza mwanzo mwisho mpaka mwamuzi aamue kupuliza filimbo kukamilisha dakika 90 hapo ndo atatoka uwanjani.

Hiyo inatokana na kipaji chake alichonacho pamoja na kutosumbuliwa na majeraha jambo ambalo ni la msingi kwa kila mchezaji na Yanga ikiwa imecheza mechi tano za ligi amecheza zote na kutumia dakika 450.

Kwa wazawa yeye ni namba moja kwa kuyeyusha dakika nyingi uwanjani akifuatiwa na Kibwana Shomari mwenye pasi moja ya bao akiwa ametumia dakika 426 kwenye mechi tano kisha ile ya tatu ipo mikononi mwa Feisal Salum ambaye ametumia dakika 425.

Kwenye mechi hizo tano ambazo alicheza alishuhudia timu yake ikishinda mechi zote na kukusanya pointi 15 huku akiokota bao moja nyavuni wakati wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa.

Kwa upande wa Fei Toto yeye ni namba moja kwa utupiaji ndani ya Yanga akiwa amefunga mabao matatu na ana pasi moja ya bao kati ya mabao tisa ambayo yamefungwa na timu hiyo.

Anafuatiwa na Fiston Mayele pamoja na Jesus Moloko kwenye suala la kutupia mabao ambapo hawa wawili kila mmoja ametupia mabao mawili huku Djuma Shaban,Tonombe Mukoko hawa wakitupia bao mojamoja na kinara wa pasi za mwisho katika timu hiyo ni Yacouba Songne mwenye pasi mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad