DEAN HENDERSON ATAKA KUSEKA NDANI YA MANCHESTER UNITED - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 12 November 2021

DEAN HENDERSON ATAKA KUSEKA NDANI YA MANCHESTER UNITED


 DEAN Henderson, kipa namba mbili wa kikosi cha Manchester United amepia mkwara kwamba anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho ikiwa hatapewa nafasi ya kuwa kipa namba moja.

Ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England kipa namba moja ni David De Gea ambaye amekuwa akifanya majukumu ya kuzuia lango la timu hiyo lisiokote mipira nyavuni.

Kwa mujibu wa Daily Mail imeelezwa kuwa kipa huyo kwa sasa anapigiwa hesabu na Klabu ya Newcastle United jambo ambalo linampa nafasi ya kusema kwamba anataka kuwa kipa namba moja ili apate sababu ya kuwaaga mabosi wake hao.

Kwa msimu huu kipa huyo amefanikiwa kucheza mchezo mmoja huku akiwa amepoteza nafasi ya kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England na dili lake ni miaka mitatu na nusu imebaki kuitumikia timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad