IKIWA uwanja wa Mkapa Novemba 11, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya DRC Congo na kufanya ile picha ya kuweza kufanya vizuri kimataifa kuishia palepale kwa kuwa hakuna matumaini tena ya kuweza kufuzu Kombe la Dunia 2022
Ilikuwa ni katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambapo Stars ilikuwa inapambana kupata pointi tatu sawa na DRC Congo huku matumaini kibao yalikuwa kwa Stars ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen kwa kuwa ilikuwa nyumbani na mashabiki wake pamoja na uwanja wa kisasa kabisa.
Kipindi cha kwanza umakini kwa safu ya ushambuliaji ya Stars inayoongozwa na Mbwana Samatta ulikuwa mdogo na kufanya wakose nafasi za wazi jambo lililowapotezea hali ya kujiamini.
Kituo kinachofuata ni Madagascar ambapo utakuwa mchezo wa mwisho kwa kundi J katika kuwanja kufuzu Kombe la Dunia.
Kwa hesabu hizo Tanzania imeondolewa katika Vita ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia kwa kuwa inabaki na pointi 7 ikiwa nafasi ya tatu huku DRC Congo ikifikisha pointi 8 ikiwa nafasi ya pili na kinara ni Benin ambaye ni namba akiwa na pointi 10.
Kim Poulsen, Kocha Mkuu wa Taifa Stars amesema kuwa timu iliadhibiwa kwa kuwa ilifanya makosa.
"Tulifanya makosa kwenye mchezo wetu ndani ya dakika sita hivyo hamna namna makosa ambayo tumeyafanya yametuponza," .

No comments:
Post a Comment