GERRARD NI KOCHA MPYA ASTON VILLA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 12 November 2021

GERRARD NI KOCHA MPYA ASTON VILLA

 


RASMI sasa Steven Gerrard ametajwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England akipewa dili la miaka miwili na nusu kwa ajili ya kuinoa timu hiyo ambayo imemchimbisha kocha wake wa zamani Dean Smith. 


Gerrard alikuwa akikinoa kikosi cha Rangers hivyo baada ya kufikia makubaliano mazuri wameridhia kocha huyo asepe na sasa anakwenda kuanza changamoto mpya.


Kazi yake ya kwanza ndani ya Ligi Kuu England inatarajiwa kuwa dhidi ya Brighton na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 20 na atakuwa na mechi tano za kuweza kukaa kwenye benchi ndani ya Novemba.


Smith ambaye alimfundisha mzawa Mbwana Samatta katika timu hiyo hakuwa na mwendo mzuri na kwenye mechi tano za Ligi Kuu England alipoteza huku mchezo wa mwisho kukaa kwenye benchi la ufundi alishuhudia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Southampton.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad