JUMLA ya mabao 13 yamefungwa kwenye mechi sita ambazo wamekutana wababe wawili KMC na Azam FC.
Klabu ya Azam FC wao wametupia mabao nane, huku KMC ikifunga mabao matano kwenye mechi za ligi.
Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zake za nyumbani ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC, Novemba 21, Jumapili.
Mchezo huounatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru ambapo timu zote zinapiga hesabu ya kusepa na pointi tatu muhimu.
Rekodi zinaonyesha kwamba Azam FC imeshinda nusu ya mechi hizo ikifanya hivyo mara tatu, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.
Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya 9 na pointi 7 baada ya kucheza mechi tano huku KMC ikiwa nafasi ya 16 na pointi mbili baada ya kucheza pia mechi tano.
No comments:
Post a Comment