ZINEDINE ZIDANE NI MWAMBA WA KAZI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 20 November 2021

ZINEDINE ZIDANE NI MWAMBA WA KAZI

 


ZINEDINE Zidane raia wa Ufaransa kwa sasa hana kazi baada ya kuondoka ndani ya Real Madrid mwishoni mwa msimu wa 2020/21 ambapo alikuwa hapo akiwa ni kocha mkuu.

Zidane amefanikiwa kutwaa mataji matatu mfululizo ya Uefa Champions League akiwa na Real Madrid ambao ni miamba ndani ya Hispania.

Rekodi zinaonyesha kwamba kwenye majukumu ya kufundisha ameweza kuongoza jumla ya mechi 167 ambazo ni dakika 15,030.

Ni jumla ya mechi 174 aliweza kushinda ikiwa ni sawa na dakika 15,660 na sare ambazo alikusanya ni 53 ambazo ni dakika 4,770.

Kichapo alikutana nacho kwenye mechi 36 ikiwa ni dakika 3,240 na ni mabao 605 aliweza kushuhudia timu yake ikifunga huku yale ya kufungwa yakiwa ni 264 na katika mechi 89 aliweza kukamilisha dakika 90 bila kipa wake kuokota bao kwenye nyavu.

Rekodi hizi ni kwenye mashindano yote ambayo amesimamia Zidane ndani ya Real Madrid alipopewa majukumu ya kuwa kocha mkuu.

Zidane mwenye miaka 49 ambaye nafasi ambayo anaicheza ni kiungo mshambuliaji ameweza kuifundisha timu moja pekee ambayo ni Real Madrid na aliweza kucheza hapo kwa mafanikio makubwa kwa msimu wa 2001/2006 na alicheza jumla ya mechi 155 na kutupia mabao 37.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad