KIUNGO SIMBA AIBUKIA AZAM FC - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 31 December 2021

KIUNGO SIMBA AIBUKIA AZAM FC




NYOTA Ibrahim Ajib leo Desemba 30 ametambulishwa ndani ya kikosi cha Azam FC kwa ajili ya kuanza changamoto mpya katika timu hiyo.


Ajib alikuwa akicheza ndani ya kikosi cha Simba lakini hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza jambo ambalo limewafanya mabosi wake kuamua kusitisha mkataba wake.


Leo mabosi wake wa Simba wamethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake kwa manufaa ya pande zote mbili.


Ni dili la mwaka mmoja amesaini ndani ya Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex. 


Amekabidhiwa jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa na Sure Boy ambaye amesaini dili la miaka miwili ndani ya kikosi cha Yanga.


Ajibu anaingia kwenye rekodi ya kuchezea timu tatu kubwa ikiwa ni Yanga,Simba na sasa Azam FC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad