ABOUTWALIB Mshery leo Desemba 29,2021 ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Yanga ikiwa ni usajili wa dirisha dogo.
Anaibuka ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar yenye maskani yake huko Morogoro.
Anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa ndani ya Yanga baada ya kuanza na Sure Boy aliyesajiliwa bure akitokea Azam FC baada ya kuomba kuvunja mkataba wake na mabosi hao wa Dar.
Ni miaka miwili amesaini Mshery kuitumikia Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, raia wa Tunisia.
No comments:
Post a Comment