LEO ni leo asemaye kesho huyo atakuwa muongo kwa kuwa wengi waliosema kesho mambo yalikuwa tofauti katika kutimiza majukumu yao unaweza kusema hivyo ama kwa namna yoyote ile lakini ukweli utajulikana baada ya dakika 90 kukamilika.
Imekuwa hivyo baada ya wengi kuisubiri siku ya leo kwa shauku kubwa na sasa ni suala la muda tu kukamilisha ile vita ya wanaume 22 Simba iliyo nafasi ya pili kufanya yao katika kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Yanga.
Itakuwa Uwanja wa Mkapa saa 11 jioni, kuelekea kwenye mchezo huo, kiungo mzawa, Zawad Mauya ambaye yupo ndani ya kikosi cha Yanga kilicho nafasi ya kwanza na pointi 19 kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amezungumza mengi.
Mauya anakumbukwa kwa kuwa aliwahi kuwa shujaa msimu wa 2020/21, Julai 3 alipomtungua kipa Aishi Manula kwa shuti lake lilizama mazima nyavuni na kuwafanya Yanga wasepe na pointi tatu jumlajumla mbele ya Simba.
Mauya amefunguka mambo mengi kuhusu mipango namna hii:-
“Tunahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza na tunatambua kwamba ligi ni ngumu nasi pia tunapambana.
Kipi kinawafanya mnakuwa bora?
“Plan ya game (mpango wa mchezo) kuwa nzuri inakuwa sababu kwetu kuweza kupata ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza. Pia benchi la ufundi ni nzuri linasoma kila mchezo na kutupa maelekezo.
“Na kumekuwa na mabadilko hasa kipindi cha pili kwa kuwa imekuwa kawaida kwa timu pinzani kutusoma kipindi cha kwanza na sisi huwa tunapambana kuweza kupata mabao ila ikitokea tukashindwa basi ni sehemu ya mchezo.
Kuelekea mchezo wenu dhidi ya Simba hesabu zipoje?
“Kila game ni pointi tatu na wao ni wapinzani wetu tunahitaji kushinda ili kupata ushindi.
“Hauwezi kuwa mchezo mwepesi utakuwa mgumu kwa sababu najua kwamba tulikutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii tukawafunga hivyo hauwezi kuwa mchezo mwepesi kuweza kuwafunga mara mbili ila sisi kama Yanga tumejiandaa kuhakikisha tunakaa katika sehemu ambayo tunaitaka.
“Mashabiki waendelee kuwa na imani na sisi kuelekea kwenye mechi hiyo ambayo itakuwa ngumu lakini sisi tupo tayari kufanya vizuri.
Uliwahi kuwafunga Simba,je ukipewa nafasi utawafunga?
“Kufunga ni nafasi hivyo mtu yoyote anaweza kufunga wakati wowote inapopatikana nafasi, siwezi kusema nitafunga lakini situation,(hali) ya game itakavyokuwa hivyo ikitokea ikapatikana nafasi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu nitafunga.
Uwepo wa wachezaji wapya katika nafasi ya viungo inaleta picha gani?
“Tunashukuru Mungu kuna vitu ambavyo vimeongezeka na na jitihada ambazo zinaonekana zinaleta matokeo mazuri.(Miongoni mwa viungo wapya ni pamoja na Jesu Moloko,Khalid Aucho).
Kuhusu Fei Toto je huwa mnazungumza nini?
“Sio kuzungumza sana mazoezini lakini inapotokea situation ya mtu kufanya vizuri mtu anapongezwa hata kwenye mechi mtu akifanya vizuri anapongezwa kwa kile ambacho anakifanya.
“Kwa upande wa kambini kila mtu huwa anakuwa na utamaduni wake lakini kwa yule ambaye anafanya vizuri kwa kuwa sisi wote ni timu moja huwa tunampongeza na sio kwenye mechi tu hata kwenye mazoezi yule anayefanya vizuri anapongezwa,” anamaliza Mauya.
No comments:
Post a Comment