LUIS ABEBA SUPER CUP AFRIKA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 24 December 2021

LUIS ABEBA SUPER CUP AFRIKA

 LUIS Miquissone nyota wa zamani wa Simba anaingia katika rekodi ya wachezaji waliosepa na taji la Super Cup baada ya timu yake mpya kushinda.



Mchezo uliochezwa Uwanja wa Al Rayyan miamba Al Ahly na Raja Casablanca walitoshana nguvu kwa kufungana bao mojamoja ambapo kwa Al Ahly Taher Mohamed alisawazisha bao dakika ya 90 ambalo Yasser Ibrahim alijifunga dakika ya 13.


Al Ahly ilishinda kwa penalti 6-5 dhidi ya Raja Casablanca. 


Ni taji la Super Cup ya Afrika Luis amelinyanyua baada ya kutoka kunyanyua makwapa na Simba akitwaa taji la Ligi Kuu Bara pamoja na lile la Shirikisho.


Luis anakuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kucheza ndani ya Ligi Kuu Bara na kubeba taji la Afrika ngazi ya klabu.


Wengine ambao wamewahi kufanya hivyo ni pamoja na Mbwana Samatta ambaye alikuwa anakipiga Simba kisha akaibukia TP Mazembe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad