AZAM FC leo imetinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 9-8 mbele ya Yanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan.
Ilikuwa ni mechi yenye ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 na hakuna timu ambayo iliweza kupata bao la kuongoza kwenye mchezo huo.
Ni mikwaju ya penalti imeamua Azam FC iweze kutinga hatua ya fainali kwa kuwa Yanga imekwama kuweza kupata ushindi leo mbele ya Azam FC.
Kutangulia kwa Azam FC kutaifanya isubiri mshindi kati ya mchezo wa Namungo FC dhidi ya Simba ili kujua nani atacheza fainali, Alhamis.
Bingwa mtetezi amevuliwa taji hilo na atashuhudia bingwa akipatikana akiwa kwenye kideo na penalti ya ushindi kwa Azam FC iliyaonza na mshambuliaji wake Idris Mbombo ilifungwa na Mudathir Yahya ambaye alianza kuwasoma Yanga akiwa nje na kushuhdia namna nahodha Bakari Mwamnyeto alvyokuwa akitimiza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment