KIKOSI cha Simba kimetinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan.
Ni mabao ya Meddie Kagere dakika ya 14 na PapeSakho dakika ya 48 yametosha kuwapa ushindi Simba.
Sasa Simba itakutana na Azam FC kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi.
Azam FC ilishinda kwenye mchezo wa fainali ya kwanza dhidi ya Yanga na ilishinda kwa penalti 9-8.
Mchezaji bora wa mchezo wa leo amechaguliwa kuwa Sakho na amekabidhiwa zawadi ya milioni moja.
Frank Mangingi wa Namungo yeye amekabidhiwa tuzo ya mchezaji muungwana na amekabidhiwa laki tatu.
Pia nyota mpya wa Simba, David Udoh aliweza kupata nafasi ya kucheza kwa muda wa dakika 8 kwa kuwa aliingia dakika ya 82 akichukua nafasi ya Kibu Dennis.
No comments:
Post a Comment