PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anawaheshimu wapinzani wake Azam FC ambao atakutana nao Uwanja wa Mkapa leo Januari Mosi, 2022 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa vigogo hawa kukutana msimu wa 2021/22 na unapigwa siku ya kwanza ya mwaka 2022.
Pablo amesema kuwa anawatambua vyema Azam FC na ni timu yenye
wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa hivyo anaamini watapata ushindani mkubwa mbele ya timu hiyo.
“Nawaheshimu Azam FC ni timu nzuri na wachezaji wake pia ni wazuri niliweza kuwafuatilia na kuona walivyocheza katika mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting, walicheza vizuri na niliona mchezaji wao mmoja anaitwa Kangwa (Bruce) alihusika kwenye mabao mengi.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutakuwa na burudani pia hasa ukizingatia ni mwaka mpya 2022 nawatakia kheri. Kuwepo kwa Ajibu (Ibrahim) ama asiwepo hilo litakuwa juu ya benchi lao la ufundi lakini ninachojua Ajibu ni mchezaji mzuri lakini alikosa nafasi,” amesema.
Ajibu kwa sasa ni mchezaji wa Azam FC baada ya kusaini dili la mwaka mmoja ameweza kuibukia huko akitokea Simba ambapo waliweza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.
No comments:
Post a Comment