SIKU MBAYA KWA NYOTA HAWA WA SIMBA WAKINYOOSHWA NA MBEYA CITY - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 17 January 2022

SIKU MBAYA KWA NYOTA HAWA WA SIMBA WAKINYOOSHWA NA MBEYA CITY




DAKIKA 90 zimekamilika na ubao wa Uwanja wa Sokoine umesoma Mbeya City 1-0 Simba na mtupiaji wa bao ni Paul Nonga dakika ya 19.

Mitambo yote ya mabao kwa Simba imegusa Uwanja wa Sokoine na mambo yakawa magumu kwao namna hii:-

Kibu Dennis

Rasta wa Simba ambaye alianza kikosi cha kwanza na kuyeyusha dakika 61.

Ndani ya dakika hizo 61 Kibu mwenye aliweza kusababisha penalti moja dakika ya 48, alipiga shuti moja lililolenga lango dk ya 7.


Chris Mugalu

Mshambuliaji wa Simba aliyeyusha dakika 90 na alikosa penalti dakika ya 48 baada ya kugongesha mwamba pia aliotea dakika ya 3.


Meddie Kagere

Ni namba moja kwa utupiaji wa mabao ndani ya Simba akiwa nayo manne na pasi moja ya bao alianza benchi na aliingia dakika ya 69, katika dakika 21 ambazo amezitumia aliweza kuotea mara moja dakika ya 89.


John Bocco

Nahodha wa Simba alitumia dakika 45 bado anamachungu kwa kuwa leo anatimiza siku ya 183 bila kufunga bao ndani ya ligi.

Alipiga mashuti mawili ambayo yalilenga lango lakini yaliishia mikononi mwa Deogratius Munish.


Ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu wa 2021/22 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad