KOMBE LA SHIRIKISHO MAKUNDI 32 BORA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 17 January 2022

KOMBE LA SHIRIKISHO MAKUNDI 32 BORA



MABINGWA watetezi wa Azam Sports Federation Cup, (ASFC) wana kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Dar City baada ya droo ya 32 bora kupangwa leo na mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya KMC v Ruvu Shooting. 



Kwa upande wa Yanga wao watacheza na Mbao FC na mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United v Mbeya Kwanza katika hatua ya 16 bora inayotarajiwa kuchezwa kati Januri 27-31 na hatua ya 16 bora inatarajiwa kuchezwa kati ya Februari 12-17.


Mechi nyingine itakuwa namna hii:-Biashara United v Mbeya Kwanza, African Lyon V Kagera Sugar,African Sports v Mtibwa Sugar, KMC v Ruvu Shooting, Baga Friends v Catamine FC.


Tanzania Prisons v Rhino Rangers,Mbuni FC v Lipuli,Pamba FC v Stand United,Azam FC v Transit Camp, Coastal Union v Top Boys, Namungo FC v Lindi United. 

Dodoma Jiji v Sumbawanga United, Polisi Tanzania v Ndanda FC na Geita Gold v Tunduru Korosho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad