Jina la Mpole halisadifu yaliyopo ndani ya kitabu...
NAKURUDISHA darasani zama zile za kitabu cha,'Kuli, Njama,Takadini nikirudi kwa kizazi cha leo kitabu cha Kilio Chetu na Watoto wa Mama Nt'ilie.
Swali moja pendwa kwamba je jina la kitabu linasadofu yaliyomo hapo pointi ni moja ndio kwa sababu imezungumzia kuhusu mfanyakazi Kuli aliyekuwa anasaka tonge kwa kuvuja jasho.
Alikuwa ni pande la jitu aliyefanya kazi kwa juhudi bila kukata tamaa licha ya kipato kuwa kipande kimoja cha fedha....
Hapo kwa Kilio Chetu tutaeleza kwamba Joti alikuwa anaonyesha namna kilio kilivyokuwa na mengine kadhalika.
Sasa turudi kwa jina la George Mpole, hapa pointi ni hapana huyu kijana yupo zake Geita katili kwa kucheka na nyavu na ametupia mabao 7 ndani ya Ligi Luu Bara.
No comments:
Post a Comment