BAADA ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wakiwa ni vinara na pointi zao 39 sasa wamebakiwa na mechi 6 ugenini.
Katika mechi 15 mzunguko wa kwanza Yanga ilicheza mechi 9 ugenini na nyumbani ilicheza mechi 6, ilishinda mechi 12, sare 3 huku ikitupia jumla ya mabao 25.
Mzunguko wa pili Yanga itacheza mechi 6 ugenini na 9 ikiwa nyumbani na ni mechi nne tu itawalazimu Yanga kusepa Dar es Salaam.
Mechi hizo ni dhidi ya Geita Gold,Biashara United ya Mara, Mbeya City ya Mbeya na Dodoma Jiji.
Mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa Dar ni dhidi ya Ruvu Shooting na Azam FC.
No comments:
Post a Comment