WAKATI ukurasa ukifungwa kwa Yanga kuimaliza KMC Uwanja wa Mkapa ulipigwa mpira wa darasani huku wachezaji wakitembezeana mikasi ya kishkaji katika msako wa pointi hizo.
Ubao ulisoma Yanga 2-0 KMC ilikuwa ni Machi 19 na waliofanya
iwe hivyo ni Matheo Anthon dk ya 39 kwa bao la kujifunga na Djuma Shaban
ilikuwa dk ya 51.
Weka kando suala la Yanga kuwa namba moja na pointi 48 hapa
Championi Jumatatu linakuletea msako ulivyokuwa kwenye mchezo huo:-
Zilitembezwa kadi za njano
Dakika 45 za mwanzo timu zote zilicheza kwa hesabu kubwa
huku kila mmoja akiwa anatafuta pa kutokea na mwamuzi wa kati Hery Sasii
hakutoa kadi yoyote mfukoni.
Kipindi cha pili hao KMC walicharuka walitembeza mabuti kama
yote na walikutana na kadi za njano ambapo jumla wachezaji watano walionyeshwa
kadi za njano.
Abdul Hassan huyu alikuwa benchi lakini alipoingia
alionyeshwa njano dk 87 baada ya kumchezea faulo Fiston Mayele kama ambavyo
ilikuwa kwa Masoud pia dk ya 83 naye alionyeshwa kadi ya njano.
Hassan Kessy ambaye alikuwa kwenye ubora pia alionyeshwa
kadi ya njano dk ya 65, Charlse Ilanfya naye alionyeshwa kadi ya njano dk ya 90
na nyota mwingine ni Kenny Ally dk ya 61 alimchezea faulo Dickson Job.
Huyu Chico kumbe mkorofi
Chico Ushindi alikuwa ni mkorofi kwenye mchezo wa juzi
ambapo alimtembezea kiwiko nyota wa KMC, Emmanuel Mvuyekule ilikuwa dk ya 48
lakini mwamuzi hakuweza kuliona hilo tukio.
Kwenye mchezo huo aliweza kutoa pasi moja ya bao ilikuwa ni
kwa Djuma Shaban baada ya kupiga kona ilikuwa dk ya 51.
Kaseja na Diarra mikono ya dhahabu
Licha ya Juma Kaseja kufungwa mabao mawili hakuna namna
anastahili pongezi kwa kuwa alifanya kazi kubwa kuokoa le michomo ya Mayele
ambaye alikuwa anahitaji kutetema ilikuwa dk ya 45 na 76 pia Chico alipiga
mashuti mawili yaliishia mikononi mwa Kaseja ilikuwa dk ya 10 na 29 kwa Yanick
Bangala ilikuwa dk ya 10 huku Djuma Shaban alifanya hivyo dk ya 13.
Diarra ilikuwa ni siku nzuri kwake kazini kwa kuwa lile
shuti la Matheo Anthon dk ya 27 ilibaki kidogo libadili usomaji wa ubao
pamoja,shuti la Awesu Awesu dk ya 76, Hassan Kabunda dk ya 80 na Ilanfya ilikuwa
dk ya 81.
Wazee wa kujenga vibanda
Vibanda kwa Yanga alikuwa ni Mayele ambaye alinaswa kwenye
mtego wa kuotea ilikuwa dk ya 34 na kwa upande wa KMC alikuwa ni dk ya 56 kwa
Kabunda.
Wazee wa mikasi
Feisal Salum kiungo huyu wa Yanga alikuwa miongoni mwa nyota
wa kwanza kucheza faulo ilikuwa dk ya 2 alimtembezea mkasi Sadala Lipangile,
Djuma Shaban alimchezea faulo Kabunda ilikuwa ni dk ya 64.
Ilanfya alikuwa na lake alimtembezea mikasi Bangala ilikuwa
dk ya 74 pia Kenny Ally yeye alikuwa na Job alifanya hivyo dk ya 61.
Makipa wote KMC ngoma droo
Makipa wote wa KMC Kaseja na Farouk Shikalo mbele ya Yanga
wote wametunguliwa mabao mawilimawili, alianza Shikalo Uwanja wa Majimaji
Songea kisha akamaliza Kaseja Uwanja wa Mkapa.
Kwenye msako wa pointi sita mbele ya Yanga KMC wameambulia
0.
No comments:
Post a Comment