MZUNGUKO wa kukamilisha duara lililoanza kuchorwa Majimaji leo unatarajiwa kukamilika kwa vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga kuwakaribisha KMC kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa Mkapa.
Mpaka sasa Yanga bado haijapoteza mchezo baada ya kucheza mechi 17 kibindoni imekusanya pointi 45 inakutana na KMC ambayo imekusanya pointi 22 zote zmecheza mechi 17.
Viongozi wa timu zote mbili wamebainisha namna hesabu zilivyo kuelekea kwenye mchezo huo ilikuwa namna hii:-
Haji Manara Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa:-“Tuna mechi ngumu na kila mchezo kwetu unakuwa ni mpango kazi wa kuweza kupata pointi tatu haina maana kwamba tunawabeza wapinzani wetu hapana.
“Mchezo wa kwanza tuliweza kupata ushindi na sasa tunakutana nao Uwanja wa Mkapa nyumbani.Mchezo wetu dhidi ya KMC kutakuwa na burudani mbalimbali za kuvutia siku hiyo hii siyo ya kukosa kabisakwa Watanzania wote na wapenda michezo.
Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanawatambua Yanga na kupoteza kwao mchezo uliopita kunawapa nguvu ya kupambana.
“Tulipoteza mchezo mbele ya Coastal Union haina maana kwamba tutakwama kushinda mbele ya Yanga, kupoteza kwetu kunatupa nguvu ya kujipanga upya ili kupata pointi tatu muhimu,”.
Mitambo ya mabao
Yanga wao ni Fiston Mayele ambaye ni mwiba kwa mabeki wengi kuonekana kukwama kumzuia akiwa ametupia mabao matano Uwanja wa Mkapa ni hapo pia aliweza kuvunja ule mwiko wa kufunga bao moja kwa kuwa alitupia mabao mawili mbele ya Kagera Sugar.
Matheo
Matheo Anthon ni moja ya mitambo ya mabao ndani ya KMC akiwa ametupia mabao manne na pasi mbili kwenye mechi 14 ambazo amecheza.
Walipoishia
Msimu huu wa 2021/22 ubao wa Uwanja wa Majimaji ulisoma KMC 0-2 Yanga hapo ndipo ambapo waliishia hivyo leo Machi 19 ule msako wa pointi tatu utaendelea kwa kuwa ngwe ya kwanza iliyopigwa Songea Yanga walitoka wanatabasamu.
Kwenye mchezo huo Fiston Mayele alifungua akaunti yake ya mabao na pasi ambapo kwa sasa ni namba moja ndani ya Yanga akiwa ametupia mabao 10 na pasi tatu za mabao kwa Feisal yeye ilikuwa ni mwendelezo wa kuwapa tabu KMC na sasa ametupia mabao manne na ana pasi tatu za mabao.
Msimu wa 2020/21
Msimu huu wa tatu kwa KMC kuwa ndani ya ligi ni mabao matano yalikusanywa na msako wa pointi sita Yanga walisepa na pointi 4 KMC ilikuwa pointi moja matokeo yao ilikuwa Aprili 10,2021, Yanga 1-1 KMC na
KMC 1-2 Yanga ilikuwa ni Oktoba 25,2020.
2019/20
Msimu wa pili ilikuwa ngoma nzito kwa timu hizi baada ya kuweza kukutana kwenye mechi mbili KMC waliweza kusepa na pointi 4 huku Yanga wakikusanya pointi moja katika msako wa pointi sita.
Ilikuwa ni Machi 12,2020 ubao wa Uwanja wa Uhuru ulisoma KMC 1-0 Yanga lilipachikwa bao pekee kwa mshambuliaji Salim Aiyee ambaye aliibuka hapo akitokea ndani ya Mwadui.
Lililikuwa ni bao lake la kwanza na la mwisho kwa staa huyo kuweza kufunga baada yah apo majeraha yalimuweka nje kisha akasepa ndani ya KMC.
Ule uliochezwa Desemba 2,2019 hakukuwa na mbabe na badala yake waligawana pointi mojamoja kwa ubao kusoma Yanga 1-1 KMC.
2018/19
Huu ulikuwa ni msimu wa kwanza kwa KMC kushiriki ligi na ni mabao manne yalikusanywa kwenye mechi mbili ambazo ziliwakutanisha wanaume hawa uwanjani.
Ilikuwa ni Machi 10,2019 ubao ulisoma Yanga 2-1 KMC hivyo kwenye msako wa pointi sita Yanga ilisepa nazo zote jumlajumla.
Bao la usiku la Fei
Oktoba 25,2018 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma KMC 0-1 Yanga, huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa KMC baada ya kupanda ligi kumenyana na Yanga na walifungwa bao la usiku lililofungwa na Feisal Salum kwa pigo huru baada ya Ally Ally kumchezea faulo Heritier Makambo.
No comments:
Post a Comment