MANULA:TUPO TAYARI KUIKABILI RS BERKANE - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 11 March 2022

MANULA:TUPO TAYARI KUIKABILI RS BERKANE

 


AISHI Manula, kipa namba moja wa Simba amesema kuwa wanaendelea vizuri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya RS Berkane.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili Machi 13 na mashabiki wamepewa nafasi ya kuweza kuuona mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Manula amesema kuwa wanatambua wapinzani wao watakuwa wanahitaji ushindi kwa kwa wao watakuwa nyumbani basi watapambana kupata ushindi.

Manula amesema:"Tunawajua vizuri wapinzani wetu na mchezo wetu uliopita tulipoteza hivyo mchezo ujao nasi tunahitaji kupata pointi tatu mihimu.

"Kila timu ni nzuri lakini kwa kuwa wanakuja nyumbani na kama ambavyo wao waliweza kutushinda kwenye mchezo tuliocheza kwao basi nasi tunahitaji ushindi," amesema.

Walipokutana nchini Morocco na RS Berkane ambayo anacheza pia Tuisila Kisinda ambaye aliwahi kucheza Yanga wameweka wazi kwamba wamekuja kusaka ushindi kwenye mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad