AZAM FC HESABU ZAKE NI KWA SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 16 May 2022

AZAM FC HESABU ZAKE NI KWA SIMBA


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa hesabu zao ni kuelekea mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba ambao ni wa mzunguko wa pili.

Katika mchezo wa kwanza Azam FC ilipoteza mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-1 Azam FC na kuwafanya matajiri hao wa Dar kuyeyusha pointi tatu muhimu.

Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa wanafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Simba.

"Tulitoka Mbeya ambapo mchezo wetu ule umeshapita na sasa tumeanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Simba ambao ni muhimu na tunahitaji matokeo.

"Kile ambacho kimepita benchi la ufundi litafanyia kazi na ambacho kwa sasa kimeanza ni maandalizi ya mchezo wetu ujao,Uwanja wa Azam Complex," amesema.

Azam FC imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City inakwenda kukutana na Simba iliyotoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Ni Jumatano ya wiki hii, Mei 18 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad