NABI ASHUSHA PRESHA YANGA ISHU YA UBINGWA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 14 May 2022

NABI ASHUSHA PRESHA YANGA ISHU YA UBINGWA

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa anajua namna ya kufanya ili timu hiyo iweze kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

 Kauli hiyo ameitoa mara baada ya wapinzani wao Simba walio nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 kupata matumaini ya kutetea ubingwa kufuatia Yanga kupata suluhu tatu mfululizo.

 

Yanga ilianza kupata suluhu dhidi ya Simba, zikafuatia nyingine mbili dhidi ya Ruvu Shooting na Tanzania Prisons.

 

 Nabi amesema kuwa ameshajua tatizo lililopo katika timu yake ambalo lilisababisha wapate suluhu kwenye michezo mitatu mfululizo ya ligi.

 

Nabi alisema kuwa mashabiki waondoe hofu juu ya ubingwa, kwani hautakwenda popote kutokana na mikakati mipya atakayokuja nayo kwa kuanzia mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

 

Aliongeza kuwa tayari amefanya kikao na wachezaji wote juzi Jumanne jioni mara baada ya kikosi hicho kuingia kambini kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam na sasa timu imeshatia timu Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad