MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Simba chini ya Kocha Mkuu Pablo Franco kesho wana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Pamba.
Huo ni mchezo wa Kombe la Shirikisho ikiwa ni hatua ya robo fainali na lazima mshindi apatikane ili kuweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali.
Mshindi wa mchezo wa kesho anatarajiwa kukutana na Yanga iliyotangulia hatua ya nusu fainali baada ya ushindi mbele ya Geita Gold kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ahmed Ally, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
Mchezo wake uliopita Simba ilikiwasha kwenye ligi ambapo ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

No comments:
Post a Comment