ZILIPIGWA PASI NYINGI SIMBA V KAGERA SUGAR UWANJA WA MKAPA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 13 May 2022

ZILIPIGWA PASI NYINGI SIMBA V KAGERA SUGAR UWANJA WA MKAPA


UKIACHANA na ushindi wa mabao 2-0 ambao Simba iliweza kupata mbele ya Kagera Sugar kupitia mabao ya Kibu Dennis mwenye mabao sita na John Bocco mwenye mabao 2,zilipigwa pasi mwanzo mwisho Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo huo ndani ya dk 90 zilipigwa jumla ya pasi 983 huku Simba wakionekana kutawala zaidi kipindi cha kwanza na Kagera Sugar walirejea kwa kasi kipindi cha pili.

Rekodi zinaonyesha kwamba kipindi cha kwanza Simba ilipiga jumla ya pasi 330 na Kagera Sugar walipiga jumla ya pasi 219.

Walipoweza kurejea kipindi cha pili Simba walipiga jumla ya pasi 289 na Kagera Sugar walipiga pasi 145.

Hivyo ndani ya dk 90 Simba iliweza kupiga jumla ya pasi 619 na Kagera Sugar iliweza kupiga pasi 364 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi.

Pablo Franco Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kipindi cha pili walirejea kufanya mapumziko kwa wachezaji wake na kupata muda wa kucheza bila presha.

Kwa upande wa Francis Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa aliwaambia wachezaji wake wacheze kwa juhudi kwa kuwa hawana cha kupoteza kwa kuwa walikuwa wamefungwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad