UWANJA wa Ilulu mchezo wa ligi umekamilika kwa wababe hawa wawili kutoshana nguvu ndani ya dakika 90 kwenye msako wa pointi tatu.
Namungo 2-2 Simba imekuwa hivyo kwa mchezo wa leo uliokuwa ni mkali ndani ya uwanja huku mashabiki wakiwa na amshaamsha mwanzo mwisho.
Mabao ya Namungo yamefugwa na Jacob Masawe dk ya 7 pamoja na Obrey Chirwa huku mabao ya Simba yakifungwa na Shomari Kapombe dk ya 43 na Kibu Dennis dk ya 79.
Timu zote zimeondoka uwanjani wakiwa wamegawana pointi mojamoja ndani ya uwanja wa Ilulu huku kipa David Kissu akiwa mmoja wa chaguo la kwanza kwa Namungo langoni.
Huu nimchezo ambao Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco aliweka wazi kwamba unampa hofu na imekuwa hivyo.

No comments:
Post a Comment