KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi kesho Mei 4,2022 kinatarajiwa kushuka uwanjani kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting.
Tayari kikosi hicho kimewasili salama Kigoma na kupokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki ambao walijitokeza jana Mei 2.
Ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya ule wa kwanza Yanga kushinda mabao 3-1 Uwanja wa Mkapa na Ruvu wao walipoteza pointi tatu.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mapokezi ambayo wameyapokea yanawapa tabasamu kubwa wachezaji pamoja na viongozi
“Ni furaha kwetu na wachezaji kwa namna ambavyo tumepokelewa hivyo tuna amini kwamba mchezo wetu utakuwa mzuri na tunahitaji kupata ushindi,”.
Yanga ni vinara wa ligi ikiwa na pointi 55 baada ya kucheza mechi 21 kwenye ligi.
Jana ilifanya mazoezi Kigoma na miongoni mwa wachezaji ambao walifanya mazoezi hayo ni pamoja na Fiston Mayele,Feisal Salum,Djuma Shaban.

No comments:
Post a Comment