UONGOZI wa Klabu ya Pamba umeweka wazi kwamba unahitaji ushindi kwenye mchezo wa leo hatua ya robo fainali mbele ya Simba.
Ikumbukwe kwamba Simba ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ambalo walitwaa hilo mbele ya Yanga kwenye fainali iliyochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.
Ikiwa Simba itapoteza mchezo wa leo itapoteza matumaini ya kutetea taji hilo na kuwapa nafasi Pamba kuweza kuleta ushindani mpya kwenye mashindano haya yenye mvuto Bongo na yanatotoa nafasi ya timu kushiriki mashindano ya kimataifa.
Kocha Msaidizi wa Pamba, Yangoo Mamboleo amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini wataingia kwa tahadhari ili kuweza kushinda.
"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunatambua kwamba ushindani mkubwa ambacho tutajitahidi ni kutafuta ushindi kwenye mchezo huo.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya mchezo huu ambao una ushindani mkubwa na kila mmoja anahitaji ushindi ambao ni muhimu na kila mmoja anahitaji ushindi.
"Kwa ambacho kipo kwa wakati huu ukweli ni kwamba kila mmoja anahitaji kushinda nasi tunahitaji ushindi washindani wetu tunawaheshimu hivyo wajitokeze kwa wingi mashabiki" amesema

No comments:
Post a Comment