KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco leo Mei 14 kimeweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikiso hatua ya robo fainali.
Pamba waliweza kujilinda ndani ya dk 15 za awali ambapo Simba walishindwa kufunga bao na Pamba pia walishindwa kuwafunga Simba.
Bao la Simba lilipachikwa na Peter Banda dk ya 45 kwenye mchezo huo baada ya mabeki wa Pamba FC kufanya makosa katika kuokoa hatari karibu na eneo la 18.
Msumari wa pili ulipachikwa na Kibu Deninis aliyepachika bao hilo ilikuwa ni dk 48 dakika 3 tu baada ya kutoka kwenye mapumziko.
Yusuph Mhilu aliweza kutupia mabao mawili kwenye mchezo wa leo ilikuwa dk ya 53 na 90 na kuwafanya Pamba kuishia hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mkapa.
Simba inakwenda kukutana na Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

No comments:
Post a Comment